Entertainment

Rolling Stone yataja Wasanii wa Kenya kwenye orodha ya nyimbo 40 za AfroPop 2022

Rolling Stone yataja Wasanii wa Kenya kwenye orodha ya nyimbo 40 za AfroPop 2022

Tovuti kubwa ya habari za burudani duniani Rolling Stone imezitaja nyimbo 3 za wasanii wa Kenya kuwa kati ya nyimbo 40 za AfroPop zilizofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2022

Kwenye orodha hiyo wimbo wa Kundi la Uncojingjong, “Dancehalling” umeshika namba 11, “Pree” ya Brooklyn Boyz nafasi ya 17 huku Mca Mca ya Wakadinali ikikamata nafasi 25 ya nyimbo 40 zilizotajwa na Tovuti hiyo.

Kwa upande wa Tanzania Marioo amekuwa msanii pekee kutoka nchini humo kuingia kwenye orodha hiyo na wimbo wake wa “Mi Amor”, aliyomshirikisha Jovial akikamata nafasi ya 39.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *