Entertainment

Nay wa Mitego adai wasanii wengi Tanzania wanatumia dawa za kulevya

Nay wa Mitego adai wasanii wengi Tanzania wanatumia dawa za kulevya

Mwanamuziki wa Hip Hop kutoka Tanzania, Nay wa Mitego amedai kuna wasanii wengi kwa sasa wanatumia dawa za kulevya ila bado hawajajulikana.

Kupitia Insta Story amesema kama kuna la kufanya kupambana na hali hiyo ni sasa kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.

“Kwenye music industry kuna tatizo kubwa la wasanii kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya, now days imekuwa too much, yaani ni fashion, yaani wanaona ndio unyamwezi” amesema.

“Ni vile tu bado hawajafikia hatua mbaya na kugundulika kufuatana na madhara ya dawa. Tahadhari kubwa kabla ya hatari, kama kuna cha kufanya ni sasa kabla ya janga” amesema Nay wa Mitego.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *