
Mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi ameamua kumpa msanii Willy Paul maua yake akiwa angali hai.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Omondi amemtaja bosi huyo wa Saldido kama mwanamuziki mwenye bidii na mwaminifu zaidi huku akihoji ni kwanini baadhi ya wakenya wanaoneekana kumchuki wakati ana kipaji cha kipekee kwenye kazi zake.
Aidha Mchekeshaji huyo amesema madalali kwenye muziki walijaribu kila njia kumshusha Willy Paul kisanaa lakini walishindwa kutokana na uthabiti wake wa kuachia nyimbo mfululizo bila kukataa tamaa.
Hata hivyo amesema msanii huyo ana uelewa mpana wa masuala ya showbiz huku akimtabiria mema kuwa huenda akawa msanii atakayetegemea kuipeperusha bendera ya Kenya kimataifa hivi karibuni