
Msanii wa Bongo Fleva, Jay Melody, ametangaza kukamilisha albamu yake mpya, ikiwa ni taktibani mwaka mmoja tangu alipoachia albamu yake ya kwanza Therapy Aprili 26, mwaka 2024.
Kupitia InstaStory kwenye mtandao wa Instagram, Jay Melody aliwafahamisha mashabiki wake kuwa albamu hiyo mpya ipo tayari, huku akiwaahidi nyimbo kuanza kusikika muda wowote kuanzia sasa. Hii inazidisha matarajio miongoni kwa mashabiki wake waliounga mkono kazi zake tangu mwanzo.
Bado hajataja jina la albamu hiyo mpya wala orodha kamili ya nyimbo, lakini matarajio ni makubwa ikizingatiwa mafanikio ya Therapy ambayo ilijumuisha nyimbo zilizotamba kwenye chati mbalimbali. Mashabiki wanasubiri kwa hamu kusikia ladha mpya kutoka kwa hitmaker huyu wa Sawa.