Sports news

Wizara ya Michezo Yatenga Milioni 300 kwa Maandalizi ya Kip Keino Classic

Wizara ya Michezo Yatenga Milioni 300 kwa Maandalizi ya Kip Keino Classic

Wizara ya Michezo imetenga shilingi milioni 300 kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya sita ya Kip Keino Classic, yatakayofanyika tarehe 31 Mei kwenye uwanja wa Ulinzi, Nairobi.

Waziri wa Michezo Salim Mvurya amesema kuwa matayarisho katika uwanja huo yanaendelea kwa kasi na yatakamilika kufikia jumamosi hii, kabla ya mbio hizo kufanyika ndani ya siku 11 zijazo.

Mwaka huu, mashindano hayo yamegawanywa katika kitengo cha kitaifa na kitengo kikuu cha kimataifa, yakitarajiwa kuvutia jumla ya wanariadha 189, wakiwemo 59 kutoka Kenya.

Mashindano haya ya siku moja yamehamishwa kutoka uwanja wa Nyayo, unaofanyiwa ukarabati kwa maandalizi ya fainali za CHAN zitakazofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Kip Keino Classic ni sehemu ya kalenda ya mashindano ya World Athletics Continental Tour Gold, na kwa mara nyingine yanatarajiwa kuangazia vipaji vya ndani na nje ya Kenya huku yakitangaza taifa hili kama kitovu cha riadha duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *