Entertainment

WINNIE NWAGI AWEKA REKODI INSTAGRAM

WINNIE NWAGI AWEKA REKODI INSTAGRAM

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Winnie Nwagi amefikisha zaidi ya followers millioni moja kwenye mtandao wa instagram.

Winnie Nwagi ambaye juzi kati aliweka wazi mpango wa kuacha muziki kutokana na skendo hakuficha furaha yake ya kuwa na wafuasi wengi kwenye mtandao huo kwani ametumia ukurasa wake wa instagram kuwapa shavu mashabiki wake kwa kumpa support kwenye shughuli zake za kimuziki kwani sio jambo rahisi Kushawishi Watu kumfuatilia Kwenye Mitandao Ya Kijamii.

Mrembo huyo amepata idadi hiyo ya followers kutokana na picha pamoja na video zenye utata ambayo wajuzi wa mambo nchini Uganda wanadai  inakwenda kinyume na maadili ya jamiii.

Hata hivyo hii inamfanya Winnie Nwagi kuingia kwenye orodha ya wasanii Kike na Watu maarufu nchini  Uganda wenye followers wengi kwenye Mtandao wa iNstagram baada ya kufikisha jumla ya Wafuasi Million moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *