
Mara baada ya kuwepo kwa kile kinachoonekana ni kubezana kwa watu waliokaribu na Diamond Platnumz na Harmonize kufuatia show za wasanii hao nchini Marekani, Mkongwe wa Bongofleva, Ray C ametaja huo kama Ulimbukeni.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Ray C amesema kwamba kumbeza harmonize na diamond kutokana shows zao za nchini marekani sio sawa kwani itakuwa vigumu kwa wasanii wa bongo kushindana na wasanii wa nchi nyingine kama Nigeria kwa mtindo huo.
Hitmaker huyo wa “Mapenzi yangu” amesema watu waache suala la kumshindanisha harmonize na diamond platinumz na badala yake wajivunie namna wasanii hao wanavyoiwakilisha vyema nchi ya tanzania kimataifa kupitia kazi zao za muziki.