Entertainment

HARMONIZE AWEKA HADHARANI TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

HARMONIZE AWEKA HADHARANI TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

Mwanamuziki wa Bongofleva na mkurugenzi wa lebo ya Konde music worldwide Harmonize ametangaza orodha ya nyimbo zitakazounda album yake ya pili, High School.

Kwa mujibu wa post ya Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram album hiyo itakuwa na jumla ya nyimbo 20.

Hitmaker huyo wa “Teacher” amewapa mashavu wasanii wageni kama rapa Sarkodie kutoka Ghana, Naira Marley kutoka Nigeria na Busiswa kutoka Afrika Kusini.

Kwa upande wa Tanzania wapo wakali kama Anjella, Sholo Mwamba na Ibraah ambao wanaikamilisha orodha ya kolabo kwenye album hiyo.

Hii itakuwa ni album ya pili kwa mtu mzima Harmonize baada ya “Afro East” iliyotoka mwezi machi mwaka wa 2020, ambayo ni miongoni mwa album kumi bora katika mtandao wa Boomplay afrika mashariki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *