
Msanii wa Swangz Avenue Azawi, amekiri kukamatwa pamoja na meneja wake kwa tuhuma za kufuja shillingi millioni 1.6 za bwenyenye mmoja nchini uganda.
Katika taarifa aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa Instagram Azawi amesema kwamba alikamatwa pamoja na meneja wake kwa madai ya kutoelewana na waandaji wa show ambayo alipaswa kutumbuiza.
Lakini pia amesema amelazimika kuweka wazi suala hilo baada ya wanablogu kuwasiliana na timu yake wakijaribu kutaka pesa kupitia njia ya ulaghai.
Kauli ya azawi inakuja mara baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa alikamatwa na polisi mwishoni mwa juma lilopita kwa tuhuma za wizi ambapo alihojiwa kwa saa kadhaa na kuachiliwa kwa dhamana.