
Siku kama ya leo Novemba 2 mwaka wa 1974 alizaliwa Staa wa muziki wa RnB na Hiphop kutoka Marekani, Nelly.
Jina lake halisi ni Cornell Iral Hayness JR. na alizaliwa huko Austin, Texas nchini Marekani ambako alianza muziki mwaka wa 1993 akiwa na kundi la Lunatics lakini mwaka wa 1999 alisaini mkataba na lebo ya muziki ya Universal Records.
Akiwa chini ya lebo ya universal mwaka wa 2000, Nelly aliachia album yake ya kwanza kama msaani wa kujitegemea iitwayo Country Grammar,album hiyo ilifanikiwa kushika namba 3 kwenye chati ya BillBoard 200 lakini pia iliweza kushika namba moja kwenye chati hiyo.
Baada ya album ya Country Grammar kuuza zaidi nakala millioni 8.4 nchini Marekani, Nelly aliachia album yake ya pili iitwayo Nellyville mwaka wa 2002, album ambayo ilikuwa na mikwaju kama Dillemma,Work it na Air Forces Ones.
Mwaka wa 2004 Nelly aliachia album mbili kwa mpigo,ambazo ni Sweat na Suit album ambazo zilifanya vizuri kwenye chati mbali mbali za muziki nchini Marekani. Album ya Sweat ilifanikiwa kushika namba mbilii kwenye chati ya Billboard 200 na kuuza ya nakala 342,000 ndani ya wiki moja tangu iachiwa kwake huku album ya Suit ikishika namba moja kwenye Billboard 200 na kuuza nakala 396,000 ndani ya wiki moja.
Mwaka wa 2008 Nelly aliachia album yake ya tano iiitwayo Brass Knuckles ikafuatwa na album yake ya sita iitwayo 5.0 album ambayo ilikuwa ngoma kama Just A Dream, ngoma ambayo ilifanikiwa kufikia viwango vya mauzo ya Platimuz mara tatu nchini Marekani.
Hata hivyo tangu aanze muziki mwaka wa 1993 Nelly ameshafanya jumla ya album saba ya muziki,EP tatu, Mixtape mbili,Singles 48 na album mbili za nyimbo ambazo zilizotoka na ambazo pia hazikutoka.
Kutokana na mafanikio yaliyopata kwenye muziki wake, Nelly ameteuliwa kushiriki kwenye tuzo mbali mbali nchini marekani na ameshinda tuzo mbili za Grammy.
Kando na muziki, Nelly ameigiza kwenye filamu nchini marekani ikiwemo Snipes ya mwaka wa 2001,The Longest ya mwaka wa 2005 na Reach Me ya mwaka wa 2014.