Gossip

Coco Jones Avalishwa Pete ya Uchumba

Coco Jones Avalishwa Pete ya Uchumba

Mwanamuziki kutoka Marekani, Coco Jones na nyota wa mpira wa kikapu kutoka NBA, Donovan Mitchell, wametangaza rasmi uchumba wao tarehe 11 Julai 2025, kupitia mitandao ya kijamii, na kuacha mashabiki wao wakiwa kwenye dimbwi la furaha.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram, wawili hao wameonesha picha na video za kipekee wakiwa kwenye mapumziko, katika video hiyo, Donovan anaonekana akipiga magoti na kumvalisha pete kimahaba Coco Jones kabla ya hatua hii, wawili hao walikuwa wakiweka uhusiano wao kwa faragha kwa takriban miaka miwili.

Baada ya taarifa hiyo ya furaha, mashabiki, marafiki na watu maarufu wamemiminika kuwapongeza, akiwemo Russell Wilson na Ciara. Ingawa tarehe ya ndoa na harusi haijatangazwa rasmi, lakini wengi wametamani wawili hawa waoane haraka iwezekanavyo.