
Wimbo wa The Kid LAROI “Stay” alioshirikiana na Justin Bieber umeandika rekodi mpya kwenye mtandao wa Spotify kwa kufikisha streams zaidi ya Billioni moja ikiwa ni kwa haraka zaidi katika historia ya mtandao huo.
Wimbo huo uliachiwa rasmi Julai 9 mwaka huu, moja kati ya singo inayopatikana kwenye mixtape yake iitwayo ‘F*ck Love’. Tayari pia umeuza jumla ya nakala milioni 2 yaani Double Platinum kwa nchini Marekani.
Stay imemfanya Justin Bieber pia kuandika historia mpya kwenye Spotify kwa kufikisha jumla ya nyimbo 9 zenye streams zaidi ya Billioni moja.