Gossip

Live Rejection! Noti Flow Amkataa Mustapha Kwenye Kipindi cha Oga Obinna

Live Rejection! Noti Flow Amkataa Mustapha Kwenye Kipindi cha Oga Obinna

Msanii mkongwe kutoka Kenya, Colonel Mustapha, amejikuta katika hali ya aibu baada ya aliyekuwa mpenzi wake, Noti Flow, kukataa pendekezo lake la ndoa wakati wa kipindi cha moja kwa moja cha Obinna TV.

Mustapha, kwa mbwembwe, alipiga goti na kumiminia Noti Flow maneno matamu mbele ya kamera. Lakini badala ya tukio hilo kuwa la kimahaba, mambo yaligeuka baada ya Noti Flow kumkataa hadharani, akieleza kuwa tayari yupo kwenye mahusiano na mtu mwingine.

Akiwa mwenye huzuni, Mustapha alisikika akilalamika kwamba huenda sababu ya kukataliwa kwake na mrembo huyo ni kazi ya mjengo aliyowahi kufanya wakati wa kipindi kigumu cha maisha yake.

Kauli yake imezua hisia mseto mitandaoni, mashabiki wengine wakimuonea huruma huku wengine wakikitafsiri kitendo hicho kama kiki ya muziki.

Kwa upande wake, Noti Flow amesema hakujua kabisa nia ya Mustapha, akisisitiza kwamba walikuwa wamealikwa tu kwenye show hiyo ili kuipromote ngoma yao mpya, na siyo kufufua uhusiano wao wa kimapenzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *