Entertainment

Shalkido Amuomba Msamaha Terence Creative Baada ya Matusi

Shalkido Amuomba Msamaha Terence Creative Baada ya Matusi

Msanii wa zamani wa kundi la Sailors, Shalkido, ameomba radhi hadharani kwa kumkosea heshima mchekeshaji maarufu Terence Creative, baada ya kumfananisha na mbwa katika kauli zake za awali.

Akizungumza baada kulamba dili la ubalozi la Dignity Furniture, Shalkido amesema maneno hayo yalitokana na maumivu na changamoto alizokuwa akipitia, lakini amejitokeza wazi kuomba msamaha, akisisitiza kwamba anajutia matamshi yake na anaamini ni wakati wa kujenga heshima na mshikamano katika tasnia ya burudani.

Kwa upande wake, Terence Creative amepokea msamaha huo kwa moyo wa upendo na akaahidi kuendelea kumuunga mkono kijana huyo, akisema kila mtu hupitia makosa na kinachohitajika ni kurekebisha mienendo.

Juzi kati Shalkido alitangaza kuwa amefilisika kiasi cha kushindwa kumudu mahitaji ya msingi. Hali hiyo ilisababisha Eric Omondi kujitokeza kumpa msaada wa pikipiki mpya pamoja na mahitaji ya kimsingi, huku pia Wakenya wenye roho ya huruma wakikusanyika kuchanga pesa za kumsaidia kurejea kwenye hali yake ya kawaida

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *