LifeStyle

Lillian Ng’ang’a Awahimiza Wanawake Kuangalia Ubora wa Wigs Wazotumia

Lillian Ng’ang’a Awahimiza Wanawake Kuangalia Ubora wa Wigs Wazotumia

Mke wa Msanii Juliani, Lillian Ng’ang’a, ameibua mjadala mitandaoni baada ya kutoa ushauri kwa wanawake kuhusiana na matumizi ya wigs.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Lillian amesema wanawake wanapaswa kupunguza matumizi ya wigs, kwani wigs zilizowekwa vibaya zinaweza kuharibu mwonekano mzuri wa make up na mavazi.

Mwanamama huyo ameeleza kuwa make up nzuri na vazi zuri vinastahili kuendana na nywele zilizotunzwa au wig iliyowekwa kitaalamu, kwani muonekano wa nywele ni sehemu muhimu ya taswira ya mwanamke.

Kauli yake imezua mjadala mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakikubaliana naye wakisema mara nyingi wigs zisizo bora huondoa mvuto, huku wengine wakimtetea wakidai kila mwanamke ana uhuru wa kujionyesha kwa namna anavyotaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *