
Rapa kutoka Marekani French Montana, hatimaye ameachia tracklist ya album yake mpya iitwayo “They Got Amnesia” inayotarajiwa kutoka Ijumaa hii, Novemba 12.
“They Got Amnesia” ina jumla ya ngoma 20 ikiwakutanisha wakali kama Rick Ross, Drake, Lil Durk, John Legend, Doja Cat ,Saweetie na wengine wengi.
French Montana ambaye mzaliwa wa Rabat, Morocco alikuwa kwenye changamoto ya kiafya kwa takribani miaka miwili akiwa ICU akiupambania uhai wake, album yake ya “They Got Amnesia” inaenda kuleta mwanga kwa kile kilichomkuta rapa huyo.
Hii inaenda kuwa album ya nne kwa mtu mzima French Montana katika muziki wake, baada ya “Montana” aliyotoka mwaka wa 2019, “Jungle Rules” ya mwaka wa 2017 na “Excuse My French” ya mwaka wa 2013.