Entertainment

Msanii Shalkidoh Kuzikwa Leo Ruiru, Kaunti ya Kiambua

Msanii Shalkidoh Kuzikwa Leo Ruiru, Kaunti ya Kiambua

Aliyekuwa msanii wa kundi la Sailors, Shalkido, anatarajiwa kuzikwa leo katika eneo la Ruiru, Kaunti ya Kiambu, wiki moja baada ya kufariki dunia kutokana na ajali ya barabarani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, rafiki wa karibu na msanii huyo enzi za uhai wake anayefahamika kama 2Mbili ametoa wito kwa wasanii na Wakenya kujitokeza kwa wingi katika mazishi hayo, akisema ni wakati wa kuonyesha upendo na umoja kwa kumpumzisha Shalkido kwenye nyumba yake ya milele.

Hii inafuatia misa ya wafu iliyofanyika jana katika kanisa la All Saints Cathedral jijini Nairobi, ambapo mamia ya watu wakiwemo wasanii, mashabiki na viongozi wa muziki walihudhuria kutoa heshima zao za mwisho.

Kifo cha Shalkido kimeacha simanzi kubwa katika tasnia ya muziki nchini Kenya, hususan miongoni mwa mashabiki wa kundi la Sailors, ambalo lilitamba miaka ya nyuma kupitia nyimbo kama Wamlambez.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *