Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nandy, ameungana na Watanzania katika kuomboleza vifo na majeruhi waliopoteza wapendwa wao kufuatia maandamano yaliyoshuhudiwa nchini hivi karibuni.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Nandy ametoa salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, na Watanzania wote walioathirika, akiwataka waendelee kuwa na subira na imani katika kipindi hiki kigumu.
Msanii huyo amesema kuwa ni wakati wa taifa kuungana kwa hekima, amani, na umoja ili kulinda thamani ya maisha na mshikamano wa kijamii.
Nandy Ameongeza kuwa Mungu awape faraja waliopoteza wapendwa wao na kuwatia nguvu kuendelea mbele kwa matumaini mapya.