Tech news

TikTok Yaondoa Zaidi ya Video Nusu Milioni Kutoka kwa Watumiaji wa Kenya

TikTok Yaondoa Zaidi ya Video Nusu Milioni Kutoka kwa Watumiaji wa Kenya

Kampuni ya TikTok imefutwa zaidi ya video 500,000 kutoka kwa watumiaji wake wa Kenya kati ya Aprili na Juni 2025, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake endelevu za kuhakikisha mazingira salama na chanya ya kidijitali.

Kwa mujibu wa ripoti yake ya Robo ya Pili ya Mwaka 2025 kuhusu Utekelezaji wa Miongozo ya Jamii (Community Guidelines Enforcement Report), jumla ya video 592,037 zilifutwa nchini Kenya kwa kukiuka miongozo ya jamii ya TikTok.

TikTok imesema mifumo yake ya ukaguzi wa mapema (proactive moderation systems) ilisaidia kutambua na kuondoa maudhui hatarishi kwa haraka, ambapo asilimia 92.9 ya video zilifutwa kabla ya kutazamwa, na asilimia 96.3 zikifutwa ndani ya saa 24 tangu kuchapishwa.

Kampuni hiyo imesisitiza kuwa hatua hizi ni sehemu ya dhamira yake ya kuhakikisha watumiaji kote duniani ikiwemo Kenya wanaendelea kujieleza kwa ubunifu huku wakihifadhi heshima na usalama katika jamii ya mtandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *