Mrembo na mtayarishaji wa maudhui Gloria Ntazola amefichua kuwa ameamua kujitenga na familia yake, akisema amechoshwa kihisia kutokana na kutothaminiwa na kukosa sapoti ya kihisia kutoka kwao.
Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Gloria alisema kuwa wengi wa ndugu zake humtafuta tu wanapohitaji pesa, lakini hawajali kuhusu hali yake au ustawi wake binafsi.
Ameeleza kuwa hali hiyo imemfanya ajihisi kuchoka, kutojaliwa na hata kuingia katika msongo wa mawazo (depression).
Gloria amesema uamuzi wake wa kujitenga si wa chuki bali ni hatua ya kujilinda kisaikolojia, ili aweze kujiponya na kuishi maisha yenye amani zaidi.
Kauli yake imezua mjadala mitandaoni, huku baadhi ya wafuasi wakimpongeza kwa kuchukua hatua ya kujipenda, wengine wakihimiza umuhimu wa familia kutambua mchango na hisia za kila mwanachama.