Entertainment

Prince Indah Achia Rasmi Albamu Mpya “Timeless Anthems”

Prince Indah Achia Rasmi Albamu Mpya “Timeless Anthems”

Mwanamuziki wa Ohangla kutoka Kenya, Prince Inda ameachia rasmi albamu yake mpya yenye nyimbo 16, iliyopewa jina “Timeless Anthems.”

Albamu hiyo, ambayo ni ya sita kwa msanii huyo, inaonyesha ukuaji na ubunifu wake katika kuchanganya miziki ya kitamaduni ya jamii ya Luo na sauti za kisasa. Indah amesema lengo lake ni kuhakikisha muziki wa Ohangla unaendelea kupaa na kuvutia hadhira pana zaidi ndani na nje ya Kenya.

Kazi ya utayarishaji wa albamu hiyo imefanywa na prodyuza Teddy B, ambaye ameshirikiana na wasanii kadhaa wakubwa nchini Kenya. Prince Indah amempongeza Teddy B kwa mchango wake mkubwa, akisema amekuwa akifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha albamu hiyo inakuwa bora na yenye thamani kwa mashabiki waliokuwa wakiisubiri kwa hamu.

Baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ni “Ngima Dhano,” “Pedeshe (Ajawa Marwa),” “Believe Me,” “Ja Herana,” “Atieno Nyar Chula,” “Mama Love,” na “I Love You.”

Albamu ya Timeless Anthems sasa inapatikana kwenye majukwaa ya muziki mtandaoni kama Spotify, Apple Music, na YouTube.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *