Sports news

Real Madrid Yazungumza na Lyon Kuhusu Kumtoa Endrick kwa Mkopo Mwezi Januari

Real Madrid Yazungumza na Lyon Kuhusu Kumtoa Endrick kwa Mkopo Mwezi Januari

Klabu ya Real Madrid inaripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na timu ya Lyon kutoka Ufaransa, kuhusu uwezekano wa kumtoa kwa mkopo mshambulizi chipukizi Endrick wakati wa dirisha la usajili la mwezi Januari.

Endrick, mwenye umri wa miaka kumi na tisa, amekuwa akipata nafasi finyu chini ya kocha Xabi Alonso, akichezeshwa kwa dakika kumi na nne pekee tangu kuanza kwa msimu huu.

Chipukizi huyo alijiunga na Real Madrid mwaka elfu mbili ishirini na nne akitokea Palmeiras ya Brazil, na katika msimu wake wa kwanza alifunga mabao saba kwenye mashindano yote.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari vya michezo barani Ulaya, mazungumzo kati ya Real Madrid na Lyon yako katika hatua za awali, lakini pande zote zinaonekana kukubaliana kwamba mkopo wa muda unaweza kumsaidia Endrick kupata muda zaidi wa kucheza.

Mchezaji huyo pia anatarajiwa kutumia nafasi hiyo kurejesha nafasi yake kwenye timu ya taifa ya Brazil, akilenga kushiriki kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao. Hadi sasa, Endrick ameichezea Brazil katika mechi kumi na nne pekee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *