Gossip

Charisma Afichua Kukusanya zaidi ya Bra 400 Kutoka kwa Mashabiki wa kike

Charisma Afichua Kukusanya zaidi ya Bra 400 Kutoka kwa Mashabiki wa kike

Msanii wa RnB kutoka Kenya, Charisma, amefichua tukio la aina yake kuhusu namna mashabiki wake wa kike wamekuwa wakionyesha mapenzi yao kwake wakati wa maonyesho yake ya muziki.

Akizungumza katika mahojiano na Zoza Podcast, Charisma amesema hadi sasa amekusanya jumla ya bra 404 zilizotupwa jukwaani wakati akiwa kwenye perfomance

Amesema kwamba hakuwahi kutarajia kuishia na idadi hiyo kubwa, lakini sasa amezizoea kama sehemu ya matukio ya burudani kwenye maonyesho yake.

Msanii huyo ametania kuwa sasa ana mpango wa kupeleka mzigo wote laundry ili ziwe safi kabla ya kufikiria hatua nyingine.

Hata hivyo Charisma amebainisha kwamba licha ya utani unaoendelea mitandaoni, kwake ni kumbukumbu ya namna mashabiki wanavyoipokea kazi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *