Entertainment

Charisma Atetea Muziki wa Kenya Baada ya Kauli kuwa Tanzania ni Bora Kimuziki

Charisma Atetea Muziki wa Kenya Baada ya Kauli kuwa Tanzania ni Bora Kimuziki

Msanii anayechipukia kwa kasi katika tasnia ya muziki nchini Kenya, Charisma, amepinga vikali madai yaliyosambaa mtandaoni hivi karibuni yakidai kwamba muziki wa Tanzania una ubora zaidi kuliko wa Kenya.

Akijibu moja kwa moja shabiki aliyeibua mjadala huo, Charisma amesema suala la ubora wa muziki halipimwi na nchi, bali linapimwa na ubunifu, uwekezaji, na jinsi msanii anavyoweza kuwafikia mashabiki wake.

Msanii huyo, amesisitiza kuwa wasanii wa Kenya wanafanya kazi kubwa na wana mitindo ya kipekee ambayo inatambulika kimataifa.

Hata hivyo amewataka mashabiki kuthamini sanaa kutoka nchi zote mbili badala ya kuanzisha migawanyiko isiyo na tija, akisisitiza kuwa ushirikiano ndio utakaoukuza muziki wa Afrika Mashariki kwa ujumla.

Kauli ya Charisma imepanua mjadala kuhusu ubora wa muziki Afrika Mashariki, huku wadau wengi wakitoa maoni tofauti kuhusu ukuaji, ushawishi na mchango wa tasnia ya muziki kutoka mataifa hayo mawili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *