Entertainment

Ringtone Arudi Mtandaoni Baada ya Ukimya wa Muda Mrefu

Ringtone Arudi Mtandaoni Baada ya Ukimya wa Muda Mrefu

Msanii wa injili Ringtone Apoko amerudi rasmi mtandaoni baada ya kipindi cha ukimya ambacho kimehusishwa na shinikizo la kesi nzito ya ardhi iliyokuwa inamkabili.

Ringtone, ambaye amekuwa miongoni mwa wasanii wenye utata mkubwa kwenye tasnia ya muziki wa injili, amesema kuwa muziki wa injili ulidorora na kupoteza mwelekeo tangu alipojiondoa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wake, kurudi kwake kunamaanisha mwanzo mpya katika kuusukuma muziki wa gospel na kurejesha kile anachokiita moto wa Mungu katika burudani.

Katika video yake ya kurejea mtandaoni, Ringtone amejitambulisha upya kama “Wazimu wa Mungu” na “Gen Z number one”, akiashiria kuwa anarudi kwa nguvu na mtazamo mpya unaolenga kuwavutia vijana na kuleta hamasa kwenye muziki wa injili.

Hata hivyo amesisitiza kuwa licha ya changamoto za kisheria na ukimya uliodumu kwa muda, amepata muda wa kutafakari na kujiandaa upya, na sasa yuko tayari kuendelea na safari yake ya muziki, huduma, na kuweka ladha mpya kwenye tasnia ya muziki wa injili nchini Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *