Mwanamuziki kutoka Uganda, Cindy Sanyu, ameibua mjadala mtandaoni baada ya kushauri mabinti kutokurukia ndoa kabla ya kutimiza malengo yao muhimu ya maisha.
Kupitia mahojiano ya hivi karibuni, Cindy amesema kwamba ndoa ni jukumu zito linalohitaji ukomavu, utulivu wa kihisia, muda wa kutosha na kujitolea, majukumu ambayo yanaweza kupoteza mwelekeo kwa mwanamke ambaye bado hajajijenga kikazi au kifedha.
Amesisitiza kuwa wanawake wengi wanaingia kwenye ndoa bila kuwa tayari, na mara nyingi huishia kushindwa kutimiza ndoto zao kutokana na majukumu na shinikizo za maisha ya ndoa.
Kwa mujibu wa Cindy, hatua ya kwanza kwa mwanamke anayetamani maisha bora ni kujijengea msingi imara kabla ya kufikiria kuolewa.