
Hatimaye rapa Kanye West na Drake wamezika tofauti zao baada ya vita vya maneno iliyokuwepo kati yao.
Inadaiwa kuwa drake na Kanye West walikuwa pamoja backstage kwenye show ya mchekeshaji “Dave Chapel na baadae walikula nae chakula cha usiku.
Kwa mujibu wa dj wa mchekeshaji Dave, DJ Trauma kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram amewashuhudia wawili hao wakimaliza tofauti zao na kupongeza kuwa ni hatua nzuri kwa muziki wa hip hop duniani.
Hivi karibuni Kanye West alijitokeza hadharani na kuomba wameliza tofauti zake na Drake ambapo alienda mbali zaidi na kuomba ushiriki Drizzy kwenye tamasha lake ambalo anatarajia kufanyika disemba 7,mwaka huu kwa lengo la kumsaidia Larry Hoover aachiwe huru kutoka gerezani ambapo anatumikia kifungo cha maisha tangu mwaka wa 1973.
Larry Hoover ambaye ni muanzilishi wa genge maarufu la kihuni na kihalifu nchini marekani liitwalo Gangster Disciples alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani kutokana na makosa mbali mbali ikiwemo mauaji, kupanga njama za uvamizi na uporaji pamoja na makosa mengine ya jinai.