Nyota mkubwa wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz, ameendelea kulipeperusha vyema bendera ya Afrika Mashariki baada ya kushiriki katika Album maalum ya mashindano ya Mataifa ya Afrika AFCON 2025 yanayoendelea nchini Morocco.
Album hiyo yenye jumla ya nyimbo kumi na mbili imewakutanisha mastaa wakubwa wa muziki kutoka mataifa mbalimbali duniani. Miongoni mwao ni Ne-Yo, Davido, French Montana, Ayra Starr, Rema, Shenseea, Jason Derulo, Mr.1, Saad Lamjarred, Akon, Yemi Alade, Innos’B, Patoranking pamoja na wasanii wengine wengi maarufu.
Katika album hiyo, Diamond Platnumz ameshiriki kwenye wimbo namba tatu unaoitwa We Are Different, akishirikiana na msanii wa Marekani Jason Derulo pamoja na msanii wa Jamaica Shenseea.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka lebo ya WCB Wasafi, wimbo huo tayari una video ambayo imekamilika na inatarajiwa kuachiwa rasmi hivi karibuni.