Sports news

Uganda Kumenyana na Tanzania Leo AFCON 2025

Uganda Kumenyana na Tanzania Leo AFCON 2025

Mataifa ya Afrika Mashariki, Uganda na Tanzania, leo yanakutana katika mechi muhimu ya pili ya Kundi C kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, yanayoendelea nchini Morocco.

Mchuano huo maarufu kama “East African Derby” umepangwa kuchezwa kuanzia saa mbili na nusu, huku timu zote mbili zikiingia uwanjani zikiwa na shinikizo la kutafuta ushindi wa kwanza kwenye mashindano hayo.

Katika mechi za ufunguzi, Uganda ilipata kipigo cha mabao 3–1 kutoka kwa Tunisia, mabingwa wa AFCON mwaka 2004, wakati Tanzania ilishindwa mabao 2–1 na Nigeria. Matokeo hayo yamezifanya timu zote mbili kubaki bila pointi, hali inayozifanya zikazane leo ili kurejesha matumaini ya kufuzu kwa hatua ya pili.

Katika mechi nyingine za leo, vigogo wa soka barani Afrika Nigeria watamenyana na Tunisia katika mchuano unaotarajiwa kuwa mkali, huku mabingwa wa AFCON mwaka 2021 Senegal wakipambana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchezo mwingine wa kusisimua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *