Mpenzi wa mtangazaji Betty Kyallo, Charlie Jones, amejitokeza na kudai kuwa yeye ndiye muasisi wa t-shirt za Mickey Mouse na Teddy Bear za 3D ambazo zimekuwa zikitrendi kwa kasi nchini Kenya msimu huu wa mwisho wa mwaka.
Kwa mujibu wa maelezo yake, wazo la T-shirt hizo lilianza kama jaribio la kuleta kitu tofauti kwenye soko la mitindo, kabla ya kushika kasi na kugeuka kuwa mtindo unaotafutwa sana nchini Kenya.
Umaarufu wa T-shirt hizo umeonekana zaidi kupitia picha na video zinazozunguka mitandaoni, zikimuonyesha mastaa na vijana wengi wakijivunia mavazi hayo kwenye sherehe, matembezi na matukio ya kijamii wakati wa sikukuu.
Hata hivyo, jambo lisilopingika ni kwamba T-shirt za Mickey Mouse na Teddy Bear 3D zimekuwa miongoni mwa mavazi yanayotamba zaidi msimu huu wa sikukuu, zikionyesha namna mitindo inavyoendelea kubadilika na kushika kasi kupitia ushawishi wa watu maarufu na mitandao ya kijamii.