LifeStyle

Akothee Aapa Kutoacha Kuwabusu na Kuwakumbatia Watoto Wake wa Kiume Licha ya Ukosoaji

Akothee Aapa Kutoacha Kuwabusu na Kuwakumbatia Watoto Wake wa Kiume Licha ya Ukosoaji

Msanii wa muziki, Akothee, ameibuka hadharani kutetea msimamo wake wa kuonyesha upendo kwa watoto wake wa kiume, akisema hataacha kuwabusu na kuwakumbatia licha ya ukosoaji unaoendelea kutoka kwa baadhi ya watu katika jamii.

Akothee amesema kuwa kuna mitazamo potofu katika jamii inayowataka wazazi, hasa akina mama, waache kuwabusu au kuwawakumbatia watoto wao wa kiume wanapokuwa watu wazima, akidai kuwa mtazamo huo unatokana na mawazo mabaya ya baadhi ya watu.

Kwa mujibu wake, yeye huwakumbatia na kuwabusu watoto wake kila anapopata nafasi, kwa sababu anaamini kuwa yeye ndiye nguzo yao kuu, na anawapa kile ambacho yeye mwenyewe hakuwahi kukipata alipokuwa anakua.

Akothee amesisitiza kuwa upendo wa mzazi, kukubalika na kujua kuwa mama anakupenda bila masharti ni msingi muhimu unaomjenga mtoto kuwa na afya nzuri ya akili. Ameongeza kuwa mtoto anayekua akijua kuwa mama yake anampenda na anamkubali hujijengea ujasiri wa maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *