Sports news

Arsenal Wasalia Kileleni EPL Licha ya Sare Emirates

Arsenal Wasalia Kileleni EPL Licha ya Sare Emirates

Vinara wa Ligi Kuu England, Arsenal, wakiwa nyumbani katika uwanja wa Emirates, wameshindwa kuibuka na ushindi dhidi ya mabingwa watetezi Liverpool katika mchezo wa kusisimua wa Ligi hiyo.

Liverpool wamefanikiwa kujikusanyia jumla ya alama nne mbele ya Arsenal katika mechi mbili walizokutana msimu huu, jambo linaloonyesha ugumu wa pambano kati ya timu hizi mbili kongwe.

Sare hiyo imeiacha Arsenal kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England kwa alama 49 baada ya mechi 21, huku Liverpool wakibaki nafasi ya nne wakiwa na alama 35 baada ya idadi sawa ya michezo.

Kwa matokeo haya, Arsenal wanaendelea kuongoza mbio za ubingwa, lakini presha kutoka kwa wapinzani wao wakuu inazidi kuongezeka, huku Liverpool wakionyesha bado wana nguvu ya kupigania nafasi za juu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *