Entertainment

Dudu Baya: Chidi Benz Alikuwa Mbeba Begi wa Profesa Jay

Dudu Baya: Chidi Benz Alikuwa Mbeba Begi wa Profesa Jay

Msanii mkongwe wa Bongoflava, Dudu Baya, amejitokeza na kuipinga vikali kauli ya Chidi Benz aliyodai kuwa alimtangulia kwenye game ya muziki, akisema madai hayo hayana msingi wowote.

Akipiga stori na Bongo24, Dudu Baya amesema hayuko kwenye level moja na Chidi Benz, akijitaja kama lejendari wa muziki wa Bongo. Ameeleza kuwa kipindi ambacho alikuwa staa mkubwa, Chidi Benz alikuwa chawa na mbeba begi wa Profesa Jay, hivyo hawezi kudai alimtangulia kimuziki.

Dudu Baya pia amedai kuwa yeye ndiye aliyempa Chidi Benz jina hilo la kisanii, wakati rapa huyo alipokuwa bado anajitafuta kimuziki na akijiita jina la rapa mkongwe kutoka Marekani Benzino. Kwa mujibu wa Dudu Baya, aliona ni vyema kumbadilishia jina ili liendane na mazingira ya muziki wa nyumbani.

Hata hivyo, Dudu Baya amesema anamuhurumia Chidi Benz, akidai kuwa bado hajarejea kwenye hali yake ya kawaida kiakili na kimuziki tangu atoke rehab. Ameongeza kuwa hali hiyo inaweza kuwa inamfanya Chidi kutoa kauli zisizo na mizani.

Dudu Baya amemtaka Chidi Benz aache kabisa kumzungumzia, akisema endapo ataendelea, huenda akalazimika kufichua mambo mengi ya zamani ambayo yanaweza kumuaibisha vibaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *