Rapa mkali kutoka Kenya, Khaligraph Jones, amewajibu kisomo wakosoaji wake wanaoendelea kutoa ushauri kuhusu kazi zake za muziki mtandaoni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Khaligraph ameposti video fupi inayoonyesha msimamo wake, akiwataka watesi wake wapunguze ushauri mwaka mpya wa 2026, huku akifanya ishara ya kuwaziba midomo.
Ingawa Papa Jones hakufafanua zaidi wala kueleza kwa kina chanzo cha kauli hiyo, video hiyo imeonekana kuwa jibu kwa wimbi la watu wanaoendelea kumkosoa na kumpangia kazi zake, hasa katika kipindi ambacho amekuwa akiendelea na miradi yake ya muziki.
Kwa ujumbe huo mfupi lakini wenye uzito, Khaligraph Jones ameonekana kuweka wazi kuwa mwaka 2026 ameamua kuzingatia kazi zake na kupuuza ushauri usiohitajika.