Msanii nyota wa Bongoflava, Harmonize, ametoa somo nzito kwa wakosoaji wa mahusiano yake na mke wake Kajala baada ya walimwengu kuendelea kuwapa ushauri tangu walipotangaza kuifufua penzi lao.
Kupitia instastory yake, Harmonize ameonekana kukerwa na hatua ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimkumbusha mke wake matukio yake ya zamani, akisema hawawezi kufuta yaliyopita kwenye maisha yao bali wameamua kuendelea na maisha yao kwa utulivu
Hitmaker huyo wa Leo, amesema wamepitia changamoto nyingi na mke wake mambo waliyoyapitia ni mengi, na kwa sasa hawako tayari kupokea ushauri wa aina yoyote kuhusu mahusiano yao.
Hata hivyo, amewataka walimwengu kuacha kutoa ushauri usiohitajika na kuacha kumkumbusha mke wake Kajala mambo ya zamani ambayo yanaweza kumkera. Amesisitiza kuwa kwa sasa wanachohitaji ni nafasi na heshima ili waendelee na maisha yao kama walivyoamua.