
Staa wa muziki wa Injili nchini Rufftone ametia nia ya kuomba ridhaa ya kugombea Useneta kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Akipiga stori na Churchil, Rufftone amepata msukumo wa kugombea useneta kutokana na kero ambazo vijana wanakutana nazo kwenye suala la kusaka ajira.
Hitmaker huyo wa “Mungu Baba” amedokeza kwamba hivi karibuni ataweka wazi jina la chama ambalo atalitumia kuwania useneta kaunti ya Nairobi.
Rufftone anakuwa msanii wa tano nchini kuweka wazi nia ya kugombea uongozi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2021 baada ya Jalang’o, Frasha, Gabu, na Prezzo.