
Hatimaye nyota wa muziki nchini Willy Paul ameachia rasmi album yake mpya aliyokuwa ikisubiriwa na mashabiki zake.
Hitmaker huyo “Lenga” amewabarki mashabiki zake na “The African Experience” album ambayo ina jumla ya nyimbo 17, ikiwa na kolabo 5 pekee kutoka kwa wakali kama Juma Jux, Eddy Kenzo,Daphne,Fik Fameica na Kelly Khumalo.
Album hiyo kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani na ina ngoma kama I Love You, My Woman,Thirty Bob, Poromoka na nyingine nyingine.
Hii ni Album ya pili kwa mtu mzima Willy Paul, baada kuachia album yake ya kwanza mwaka wa 2020 iitwayo songs of solomon ikiwa na jumla ya mikwaju kumi ya moto.