
Staa wa muziki kutoka Nigeria, Rema’ ameamua kumtolea uvivu Dj Neptune kwa kitendo cha kwenda kinyume na makubaliano yao hii ni baada ya kuachia na kuuweka kwenye album yake mpya wimbo waliofanya zamani bila kufuata muongozo kutoka kwa uongozi wake.
Rema ametumia ukurasa wake wa twitter akimtaka Dj Neptune auondoe wimbo namba nne kutoka kwenye album hiyo uitwao “For You” ambao ndio walifanya pamoja, ikiwa ni baada ya kutoka rasmi kwa album hiyo mpya ambayo ni “Greatness”.
Rema amemtaka Dj Neptune auondoe wimbo huo kabla hawajawa maadui. Hata hivyo Dj Neptune hajajibu chochote kufuatia malalamiko hayo kutoka kwa Rema.