
Mke wa msanii Bahati, Diana Marua amegeukia kufanya muziki baada ya kutamba kwenye mitandao ya kijamii kwa miaka mingi.
Diana ambaye ni mama wa watoto wawili ameachia rasmi wimbo wake wa kwanza wenye mahadhi ya HipHop ambao kaupa jina la “Hatutaachana”.
Diana Marua ambaye anafahamika kwa jina la usanii kama Diana B anajiunga kwenye orodha ya mastaa ambao hapo awali walitambulika kama washawishi wakubwa kwenye mitandao ya kijamii na baadae wakageukia kufanya muziki