Entertainment

MASTER PIECE AMVUA NGUO WILLY PAUL

MASTER PIECE AMVUA NGUO WILLY PAUL

Msanii wa muziki nchini Masterpiece amefunguka juu ya ugomvi wake na msanii Willy Paul.

Akipiga stori na Mungai Eve, Masterpiece amesema hana ugomvi wowote na msanii huyo ila aache kiburi kwa wasanii wenzake kama anataka kufika mbali kimuziki.

Hitmaker huyo wa “Why lie” amehamua kumtolea uvivu willy paul kwa kusema kwamba album yake mpya “African Experience” ni album mbovu kuachiwa kwa mwaka huu wa 2021 kwani bosi huyo wa Saldido alikosa ubunifu wa kutoa muziki mzuri.

Ikumbukwe Masterpiece na Willy Paul hajakuwa na maelewano mazuri katika siku za hivi karibuni kwani mwaka wa 2020 walirushiana maneno makali kwenye mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *