Entertainment

VANESSA MDEE AANIKA DENI ANALODAI BENKI YA STANDARD CHARTED TANZANIA

VANESSA MDEE AANIKA DENI ANALODAI BENKI YA STANDARD CHARTED TANZANIA

Staa wa muziki wa Bongofleva Vanessa Mdee,  ameanika kutomaliziwa malipo yake na benki ambayo aliifanyia kazi kama balozi.

Vee Money ametumia ukurasa wake wa Twitter kueleza hilo pamoja na kuwataka wasanii na watu maarufu Afrika mashariki kutoruhusu makampuni kuwatumia kwa maslahi yao binafsi.

“Artists na watu maarufu Tanzania please don’t let these corporate companies take advantage of you. Mpaka leo lile benki halijamaliza kunilipa. Japo kiukweli ni benki bora but wameona wajikaushe. Yote kheri.” – ameandika Vannesa Mdee.

Ikumbukwe, Vanessa Mdee alitangazwa kuwa Balozi wa Benki ya Standard Chartered nchini Tanzania, mwezi Februari mwaka wa 2019.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *