Entertainment

AKOTHEE AFUNGUKA CHANZO CHA MWILI WAKE KUONGEZEKA

AKOTHEE AFUNGUKA CHANZO CHA MWILI WAKE KUONGEZEKA

Staa wa muziki nchini ambaye pia ni mfanyabiashara, Akothee amefunguka kinachosababisha mwili wake kuongezeka na kumfanya kuonekana mnene kuliko kawaida.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, ameeleza kuwa; “Usikutane na mimi kisha uanze kuniambia nilivyonenepa. Nina shida ya kiafya ambayo imefanya mwili wangu unenepe kwa sababu ya kukosa usingizi kutokana na maumivu.”  

Akothee anasema anaogopa kulala kwa sababu anajua akiamka atakuta sehemu za mwili wake zimekufa ganzi hasa vidole vya mikono.

Pia amemzungumzia rafiki yake wa karibu ambaye anachukulia kuugua kwake kama mzaha akisema anajisingizia tu kuwa mgonjwa.

“Sijui cha kumwambia. Kwani nipo katika shule ya bweni ndio nijisingizie ugonjwa ili nipate fursa ya kwenda nyumbani? Alishangaa Akothee.

Mwanamuziki huyo ameamua kuweka wazi juu ya afya yake hii ni baada ya kuwa anapata maoni yanayomtaka apungue kutoka kwa baadhi ya mashabiki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *