
Rapa kutoka nchini Marekani French Montana ametangaza kumalizika kwa bifu yake na 50 Cent.
Kwenye mahojiano na Podcast ya Drink Champs, Montana amesema bifu hiyo iliisha baada ya kutazama series ya “Black Mafia Family” ambayo inaruka kupitia Starz.
Sina tatizo na 50 Cent baada ya kuachia BMF. Hii ndio series yangu bora, ndio kazie yake bora pia.” alisema Montana.
Baada ya kauli hiyo, 50 Cent ameibuka kwenye mtandao wake wa instagram na kuunga mkono kilichosemwa na French Montana kwa kusema hilo ni jibu zuri, huku akitania kwamba haikumbuki kabisa bifu hiyo.
Bifu lao lilianza mwaka wa 2019 baada ya 50 Cent kumtuhumu French Montana kwamba alinunua gari feki aina ya Bugatti lakini pia amenunua streams za wimbo wake wa “Writing on the Wall” aliowashirikisha Post Malone na Cardi B.
French alijibu mashambulizi kwa ku-post picha iliyotengenezwa (photoshopped) ya 50 Cent akimpiga busu Eminem.