
Video vixen kutoka nchini Tanzania ambaye anatambulika kama msanii kwa sasa Gigy Money amedai kuwa msanii Harmonize si msanii mkubwa kwake bali amemzidi na kumpita mafanikio tu.
Gigy Money amefunguka hayo akijibu swali kuhusu kufanya kazi na mwanamuziki huyo kutoka KondeGang katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, kwa kudai kuwa mtu hawezi badilisha mtazamo wake, kwani anajua msanii huyo kabla hata hajaanza muziki kutoka record label ya WcB, hivyo ni msanii aliyempita kwa mafanikio lakini si mkubwa kwake.
Aidha mwanadada huyo ameongeza kuwa bado hajafikiria kufanya kazi yoyote na msanii huyo kwani anamuona ni msanii wa kawaida kwake