
Mkali wa muziki nchini Chikuzee amekanusha madai yaliyoibuliwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa ni mtumizi wa madawa ya kujichibua ngozi.
Chikuzee amewajibu mashabiki hao kwa kusema kuwa utumizi ya maji masafi na kula matunda kwa wingi ndio sababu iliofanya yeye kupata mabadiliko makubwa ya Ngozi.
Hata hivyo amewataka mashabiki hao kuangazia mziki anaofanya na kukoma kuangazia rangi ya ngozi yake.
Kauli hiyo ya mtu mzima Chikuzee inajiri baada ya kuachia picha mitandaoni ilioonyesha mabadaliko makubwa ya rangi ya ngozi yake kwa kiasi kikubwa.