Entertainment

G-NAKO KUWABARIKI MASHABIKI NA MINI TAPE IJUMAA HII

G-NAKO KUWABARIKI MASHABIKI NA MINI TAPE IJUMAA HII

Rapa mahiri kutoka kundi la Weusi, G-Nako ametangaza ujio wa Mini Tape yake inayokwenda kwa jina la “Kitimoto” ambayo itatoka Ijumaa hii, Desemba 10, mwaka wa 2021.

Mkali huyo ambaye jina lake halisi ni George Mdemu, huu unakuwa ujio wake mpya baada ya miezi tisa kupita bila ya kuachia kazi zake mwenyewe kama solo artist.

Mara ya mwisho kuachia kazi ilikuwa Machi 4, mwaka wa 2021 alipoachia wimbo wake uitwao “Jiachie”.

Utakumbuka Machi 12, 2021 kundi la Weusi waliachia albamu hiyo ya kwanza yenye nyimbo 14 ambapo walishirikisha wasanii wawili tu ambao ni Malkia wa Taarabu nchini, Khadija Kopa na Jojo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *