Entertainment

MULAMWAH AFUNGA LEBO YAKE YA MUZIKI

MULAMWAH AFUNGA LEBO YAKE YA MUZIKI

Mchekeshaji David Oyando maarufu kama Mulamwah ametangaza kufunga lebo yake ya muziki, kwa kile alichokitaja kuwa anapokea chuki nyingi kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, baada ya kuachana na baby mama wake Carol Sonie.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mchekeshaji huyo amesema hataki kumtia hatiani msanii wake Vall Wambo kutokana na matusi anayopokea kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii na ndiyo maana ameamua kufunga lebo yake ya muziki iitwayo ‘Mulamwah Entertainment’.

Ameenda mbali zaidi na kumhakikishia msaini wake Wambo, kuwa nyimbo zote alizozifanya akiwa chini ya lebo hiyo ni zake, ijapokuwa nyimbo hizo hazipatikani kwenye mtandao wa YouTube.

Ikumbukwe mwezi Oktoba, Mulamah alimsajili Vall Wambo kwenye Lebo yake mpya kama msanii wake wa kwanza ambapo aliachia wimbo wake wa kwanza uitwao Dawa ya Baridi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *