LifeStyle

KANYE WEST KURITHI NAFASI YA VIRGIL ABLOH KAMA MKURUNGEZI WA LOUIS VUITON

KANYE WEST KURITHI NAFASI YA VIRGIL ABLOH KAMA MKURUNGEZI WA LOUIS VUITON

Rapa kutoka Marekani Kanye West anatajwa kama mrithi wa nafasi ya marehemu Virgil Abloh kama Mkurugenzi wa ubunifu kwenye kampuni ya Louis Vuitton.

Jarida la The Sun limeripoti kwamba Kifo cha Abloh kilimgusa sana YE kutokana na ukaribu waliokuwa nao kwa zaidi ya miaka 12, hivyo kukaa kwenye kiti chake pale Louis Vuitton anajihisi kama atakuwa amelipa deni la urafiki wao kwa kukamilisha ambacho alikuwa amekiacha.

Virgil Abloh alifariki dunia Novemba 28 mwaka huu kwa ugonjwa wa Saratani ambao alikuwa akipambana nao kwa miaka miwili. Abloh alikutana na YE mwaka 2009 wakati wakifanya kazi kwenye kampuni ya Fendi mjini Roma nchini Italia.

Mwaka 2018 marehemu Abloh alitangazwa kuwa Mkurugenzi wa ubunifu upande wa mavazi ya Kiume kwenye kampuni ya Louis Vuitton.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *