
Hatimaye msanii wa muziki wa dansi mwenye asili ya Congo Christian Bella amekata kiu ya mashabiki zake na EP mpya inayokwenda kwa jina la Sweet Melody.
Christian Bella ameamua kuwa surprise mashabiki zake kwa kuachia EP hiyo mpya yenye jumla ya mikwaju 6 ya moto huku ikiwa na kolabo 3 ambazo amewashirikisha wakali kama Champagne, Isha Mashauzi na CBO Music.
Sweet Melody EP ina nyimbo kama Umeniteka, Gaga, Teamo, Ringa, Waone Gere na Wenge. Hata hivyo Christian Bella amesema ameachia Happy Hour EP kama zawadi ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya.
Hii ni kazi ya kwanza kwa mtu mzima Christian Bella kwa mwaka wa 202 Β na inapatikana exclusive kwenye Digital Platforms zote za kusambaza muziki duniani ikiwemo Boomplay.