
Msanii wa Bongofleva, Diamond Platnumz amesema ni vigumu kwa watu sasa kumfahamu mpenzi wake kwani hapatikana hata google.
Akizungumza katika behind the scenes ya video ya wimbo wake ‘Unachezaje’, Diamond amesema viatu alivyovivaa ameletewa na mpenzi wake ambaye yupo nje ya Tanzania.
“Hii Bottega original, nimeletewa na mke wangu, baby kaniletea kutoka sehemu tu, hazitoki Tanzania, nje. Ni zawadi kutoka kwa mpenzi wangu. Bottega halisi!” alisema Diamond.
Diamond ambaye amehusishwa kutoka kimapenzi na Zuchu, amewahi kuwa na mahusiano na warembo kama Penny, Wema Sepetu, Zari The Bosslady, Hamisa Mobetto na Tanasha Donna.
Utakumbuka tangu Machi mwaka wa 2021 alipoachana na Tanasha Donna kutoka Kenya, Diamond hajaweka wazi mahusiano yake ingawa kumekuwa na tetesi nyingi zikimuhusu.